Mwakilishi wa Mji Mkongwe (CUF), Ismail Jussa Ladhu ametaka kuvunjwa kwa Muungano. Nimetuma maoni yafuatayo kwenye gazeti la Mwananchi.
Maoni ya mwakilishi wa CUF Jussa yanabidi ya kemewe sio tu na chama chake
bali na watu wote wa Tanzania Bara na Visiwani. Maoni ya uchochezi
yasiyo na msingi hayapaswi kuvumiliwa. Kiongozi yeyote ambaye anasimama
mbele ya watu na kusema muungano haupaswi kuwepo ilhali takwimu za
utafiti wa Tume ya Katiba inaonyesha idadi kubwa ya watu wa Tanzania
wanataka muungano uwepo anapaswa kutoltiliwa maanani. Chama cha CUF
kinapaswa kutoa tamko na kuhusiana na kauli ya Bw. Jussa! Watanzania
wameainisha mstakabali wao kupitia rasimu ya awali ya Katiba. Sasa
mjadala sio uwepo wa muungano bali mfumo na uthabiti wa muundo wa
muungano. Tusikubali watu walio na maslahi binafsi ya uongozi
kuturudisha nyuma.
No comments:
Post a Comment