Nicodemus Minde, Nairobi
Kiu ya
ukata wa ligi kuu Kenya kwa timu ya Gor Mahia inaendelea. Ni miaka 18 tangu
wautwae ubingwa wa Kenya. Kiu hii ilikua ikatwe kwa Gor kuifunga Thika United
kwani walikua wanaongoza ligi kwa pointi moja. Licha ya hilo, Gor walikua
walikuwa wanakamilisha ratiba ya mechi kwenye uwanja wao wakihistoria wa City
Stadium na kwa maoni ya mashabiki wengi walikua wanakutana na timu ambayo
isingewaumiza kichwa hata kidogo. Timu ya Thika United sio timu ambayo Gor
Mahia wangeihofia sana. Isitoshe walikuwa washaifunga AFC Leopards na Tusker
ambazo nazo zilikua zinawania ubingwa. Kibarua cha kuifunga Thika United
kilikuwa kidogo sana ukilinganisha na mtihani wao dhdi ya AFC Leopards na
Tusker. Mashabiki wa Gor walitamba kwamba kiu ya ubingwa ingeisha kwa kuifunga
Thika United kiulaini kwenye uga wa City. Lakini wapi! Gor walilazimisha sare na
timu ‘dhaifu’ ya Thika United na Tusker wakashinda hivyo kutetea ubingwa.
Zipate sababu tano za Gor Mahia kukosa ubingwa.
1. 1. Presha ya Mechi
Licha
ya kuongoza ligi na kuingia katika mechi ya mwisho ya ligi dhidi ya Thika
United na mmoja wa mastraika hatari, Danny Ssserukuma, Gor Mahia walikuwa na
presha kubwa sana. Ni miaka kumi na saba tangu Gor watwae ubingwa wa ligi kuu
Kenya. Licha ya matokeo mazuri mwishoni mwa ligi, Gor Mahia walijikuta na
presha nyingi. Kulikua na presha ya mashabiki, presha ya kuleta ubingwa baada
ya miaka mingi ya ukata, presha yakurudisha hadhi ya timu ya Gor Mahia n.k.
Ilikuwa ni wazi kwamba mambo haya yalicheza kwenye saikolojia ya wachezaji wa
Gor hivyo lukosa ubingwa.
2. 2.Kupanick kwa Logarusic
Kocha
wa Gor Mahia alikuwa na presha nyingi kwenye mechi ya mwisho dhidi ya Thika
United. Alikua hajatulia hata kidogo. Alikua anamhemko na hakutulia kwenye
benchi. Alifanya mambo kwa pupa sana. Dhihirisho tosha ni pale alipofanya
mabadiliko mapema alipoona mabo hayaendi sawa kwenye kipindi cha kwanza. Licha
ya mabadiliko hayo kuleta uhai na afueni kidogo, kipindi cha pili pia alifanya
mabadiko ya pupa mno. Mechi kama hizi, kocha anapaswa kutulia kwenye benchi
akitoa mawaidha kidogo kwani wachezaji wanajua fika shughuli pevu
inayowakabili.
3. 3. Matano kucheza “Mind-games”
Kocha
wa Manchester United Sir Alex Ferguson ndio mtaalamu wa kuwachezea makocha wa
timu pinzani mchezo wa akili (mind-games). Mchezo huu unasaidia sana kuvuruga
mipango ya kocha wa timu pinzani. Kocha wa Tusker Robert Matano aliulizwa baada
ya kufungwa na Gor Mahia mstakabali wa ligi. Alijibu kwa maneno machache na
kusema ligi bado haijaisha. Hizo zilikuwa wiki mbili zilizopita. Aliendelea
kusisitiza kauli hii lich ya kuwa Gor Mahia kuwa kwenye nafasi nzuri ya
kushinda ligi zaidi ya timu yake. Alipohojiwa tena kwenye runinga ya Super
Sports, Matano aliendelea kusisitiza kwamba bado ligi ni mbichi na timu yake
itapambana hadi mwisho. Msimamo huu uliiweka Gor Mahia kwenye presha kubwa,
wakijua wakiteleza tu, ligi inawaponyoka. Gor walipoteleza kwa kulazimishwa
sare na Tusker walihifadhi taji lao kwa kuibamiza City Stars.
4. 4. Mashabiki kujiamini mno
Mashabiki
wa Gor Mahia wanatambulika kwa tambo zao. Wanambwebwe nyingi sana. Wanaipenda
timu yao sana. Ni jambo zuri sana kwa timu kuwa na mashabiki wa namna hii.
Wachezaji wanapata motisha kubwa kutokana na ushabiki huu. Kabla ya mechi yao
na Thika United, mashabiki wa Gor walionekana jijini Nairobi wakiwa wameandika
jezi zao “Mabingwa 2012”. Wengi wao waliweka nembo ya kombe la ligi kwenye mashati
yao huku wengine wakibeba kombe bandia la ligi. Sio vibaya kujiamini.
Inaeleweka kwenye soka, lakini kujiamini huku kuliwatia wachezaji presha kubwa
sana. Ndio hivo, baada ya mechi wengi walijawa na majonzi na simanzi kubwa
baada ya Gor kuukosa ubingwa.
5. 5. Soka safi la Thika United
Wengi
wanachambua udhaifu wa Gor kwenye mechi yao ya mwisho na wanaisahau Thika
United. Thika United walicheza bila presha yoyote. Walitandaza soka safi na la
kuburudisha. Walipiga pasi nyingi na kuwanyima Gor mpira kwa muda mrefu.
Hawakupaki basi kama timu nyingi hufanya zinavyocheza na Barcelona. Walionana
vema sana. Walipotangulia kufunga goli ndipo mpira wa ukahimarika zaidi.
Walipiga pasi fupi fupi huku mastraika wao wakiisumbua ngome ya Gor Mahia mara
kwa mara. Walipiga mashambulizi mengi ya kushtukizia pia. Kwa mpira huu, Gor
walishindwa kuivunja ngome ya Thika.