Skip to main content

Sababu Tano za Gor Mahia kuukosa ubingwa

Nicodemus Minde, Nairobi
Kiu ya ukata wa ligi kuu Kenya kwa timu ya Gor Mahia inaendelea. Ni miaka 18 tangu wautwae ubingwa wa Kenya. Kiu hii ilikua ikatwe kwa Gor kuifunga Thika United kwani walikua wanaongoza ligi kwa pointi moja. Licha ya hilo, Gor walikua walikuwa wanakamilisha ratiba ya mechi kwenye uwanja wao wakihistoria wa City Stadium na kwa maoni ya mashabiki wengi walikua wanakutana na timu ambayo isingewaumiza kichwa hata kidogo. Timu ya Thika United sio timu ambayo Gor Mahia wangeihofia sana. Isitoshe walikuwa washaifunga AFC Leopards na Tusker ambazo nazo zilikua zinawania ubingwa. Kibarua cha kuifunga Thika United kilikuwa kidogo sana ukilinganisha na mtihani wao dhdi ya AFC Leopards na Tusker. Mashabiki wa Gor walitamba kwamba kiu ya ubingwa ingeisha kwa kuifunga Thika United kiulaini kwenye uga wa City. Lakini wapi! Gor walilazimisha sare na timu ‘dhaifu’ ya Thika United na Tusker wakashinda hivyo kutetea ubingwa. Zipate sababu tano za Gor Mahia kukosa ubingwa.
1.       1. Presha ya Mechi
Licha ya kuongoza ligi na kuingia katika mechi ya mwisho ya ligi dhidi ya Thika United na mmoja wa mastraika hatari, Danny Ssserukuma, Gor Mahia walikuwa na presha kubwa sana. Ni miaka kumi na saba tangu Gor watwae ubingwa wa ligi kuu Kenya. Licha ya matokeo mazuri mwishoni mwa ligi, Gor Mahia walijikuta na presha nyingi. Kulikua na presha ya mashabiki, presha ya kuleta ubingwa baada ya miaka mingi ya ukata, presha yakurudisha hadhi ya timu ya Gor Mahia n.k. Ilikuwa ni wazi kwamba mambo haya yalicheza kwenye saikolojia ya wachezaji wa Gor hivyo lukosa ubingwa.
2.      2.Kupanick kwa Logarusic
Kocha wa Gor Mahia alikuwa na presha nyingi kwenye mechi ya mwisho dhidi ya Thika United. Alikua hajatulia hata kidogo. Alikua anamhemko na hakutulia kwenye benchi. Alifanya mambo kwa pupa sana. Dhihirisho tosha ni pale alipofanya mabadiliko mapema alipoona mabo hayaendi sawa kwenye kipindi cha kwanza. Licha ya mabadiliko hayo kuleta uhai na afueni kidogo, kipindi cha pili pia alifanya mabadiko ya pupa mno. Mechi kama hizi, kocha anapaswa kutulia kwenye benchi akitoa mawaidha kidogo kwani wachezaji wanajua fika shughuli pevu inayowakabili.
3.      3. Matano kucheza “Mind-games”
Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson ndio mtaalamu wa kuwachezea makocha wa timu pinzani mchezo wa akili (mind-games). Mchezo huu unasaidia sana kuvuruga mipango ya kocha wa timu pinzani. Kocha wa Tusker Robert Matano aliulizwa baada ya kufungwa na Gor Mahia mstakabali wa ligi. Alijibu kwa maneno machache na kusema ligi bado haijaisha. Hizo zilikuwa wiki mbili zilizopita. Aliendelea kusisitiza kauli hii lich ya kuwa Gor Mahia kuwa kwenye nafasi nzuri ya kushinda ligi zaidi ya timu yake. Alipohojiwa tena kwenye runinga ya Super Sports, Matano aliendelea kusisitiza kwamba bado ligi ni mbichi na timu yake itapambana hadi mwisho. Msimamo huu uliiweka Gor Mahia kwenye presha kubwa, wakijua wakiteleza tu, ligi inawaponyoka. Gor walipoteleza kwa kulazimishwa sare na Tusker walihifadhi taji lao kwa kuibamiza City Stars.
4.      4. Mashabiki kujiamini mno
Mashabiki wa Gor Mahia wanatambulika kwa tambo zao. Wanambwebwe nyingi sana. Wanaipenda timu yao sana. Ni jambo zuri sana kwa timu kuwa na mashabiki wa namna hii. Wachezaji wanapata motisha kubwa kutokana na ushabiki huu. Kabla ya mechi yao na Thika United, mashabiki wa Gor walionekana jijini Nairobi wakiwa wameandika jezi zao “Mabingwa 2012”. Wengi wao waliweka nembo ya kombe la ligi kwenye mashati yao huku wengine wakibeba kombe bandia la ligi. Sio vibaya kujiamini. Inaeleweka kwenye soka, lakini kujiamini huku kuliwatia wachezaji presha kubwa sana. Ndio hivo, baada ya mechi wengi walijawa na majonzi na simanzi kubwa baada ya Gor kuukosa ubingwa.
5.      5. Soka safi la Thika United
Wengi wanachambua udhaifu wa Gor kwenye mechi yao ya mwisho na wanaisahau Thika United. Thika United walicheza bila presha yoyote. Walitandaza soka safi na la kuburudisha. Walipiga pasi nyingi na kuwanyima Gor mpira kwa muda mrefu. Hawakupaki basi kama timu nyingi hufanya zinavyocheza na Barcelona. Walionana vema sana. Walipotangulia kufunga goli ndipo mpira wa ukahimarika zaidi. Walipiga pasi fupi fupi huku mastraika wao wakiisumbua ngome ya Gor Mahia mara kwa mara. Walipiga mashambulizi mengi ya kushtukizia pia. Kwa mpira huu, Gor walishindwa kuivunja ngome ya Thika.

Comments

Popular posts from this blog

Speculating Magufuli’s absence at Uhuru Kenyatta’s Inauguration

29 November 2017 As I drove on the Thika Superhighway on the weekend before Uhuru Kenyatta’s inauguration on Tuesday, the road was decorated with flags of different countries. At the foot-bridge next to National Youth Service (NYS) Headquarters, the Tanzanian flag flew sublimely. Other flags including the Nairobi City Council flag decorated the Thika Superhighway that headed towards Kasarani, the venue of the inaguration. The Office of the Government Spokesman in Tanzania, had on 24 November issued a press statement saying that President John Magufuli would attend Mr. Kenyatta’s swearing in on 28 November. Days before Mr. Kenyatta’s inauguration, NASA leader Raila Odinga, a close friend to Mr. Magufuli flew to Zanzibar, where it is reported that the two met. Mr. Odinga’s trip to Zanzibar which came a few days after he jetted back to Nairobi from an overseas trip sparked debated and controversy. On the inauguration day, Tanzania’s State-House issued a press release saying that Vice Presi…

Comment: The Politics of Party Defection in Tanzania

Political party defection is a sign of unstable party democracy and/or jockeying for political positions. Defections happen from ruling party to the opposition and from the opposition to the ruling party. In African fledgling democracies, party defections are not about ideology or philosophic underpinnings. Party switching in many African states is largely driven by ethno-demographic and religious factors. These factors have also informed political party formation. Party switching is also a strategic political manoeuvring. Despite Tanzania boasting of national parties, political party strength is largely regional. We're now witnessing a surge in party defections from across the parties.
The defection of former PM Edward Lowassa from CCM to Chadema in 2015 was monumental, especially it coming just before a general election. The election season several high-profile defections. Defections from a dominant ruling party like CCM to the opposition is always huge. CCM's single party d…