Saturday, 22 December 2012

Chadema Yateka jiji la Arusha, Lema asema Arusha ni kitovu cha mabadiliko Tanzania

Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimetoa rai kwamba Arusha ndio chimbuko la mabadiliko Tanzania. Mbunge aliyerudishwa baada ya kuenguliwa Godbless Lema amesema mwamko wa wananchi wa Arusha ni taswira kwamba wakati wa mapinduzi umefika. Mwaka wa 2013 umetajwa na viongozi wa Chadema kama ni mwaka wa kazi na hawatalala. Baada ya Lema kushinda kesi yake, viongozi wa Chadema wakizungumza kwenye hafla ya kumkaribisha Lema kwenye viwanja vya Kilombero, Arusha wamesema kwamba watazunguka nchi nzima kuwahamasisha wananchi kuhusu maovu ya CCM. 

No comments:

Post a Comment