Sunday, 3 February 2013

Hollande atua Timbuktu: Aja kuwapa sapoti wanajeshi wake


Kupitia wahisani
Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, amewasili mjini Timbuktu, Mali, ambako wanajeshi wa Ufaransa na Mali waliukomboa kutoka kwa wapiganaji wa Kiislamu siku sita zilizopita.

Waandishi wa habari wa kimataifa huko anasema Bwana Hollande amepokelewa kwa shangwe kwa sababu watu wa Timbuktu wamepumua kuwa utawala wa kikatili umemalizika. Kiongozi huyo wa Ufaransa - akifuatana na mawaziri kadha - anafanya ziara ya siku moja nchini Mali ili kuwaunga mkono wanajeshi wake. 

Akizungumza mjini Paris kabla ya kuondoka, Bwana Hollande alieleza azma ya safari yake:

"Nakwenda Mali kuwaambia wanajeshi wetu jinsi tunavyowaunga mkono na kuwapa moyo na kwamba tunawaonea fahari. Nakwenda Mali kuwezesha majeshi ya Afrika yajiunge nasi haraka iwezekanavyo, na kuwaambia kwamba tunawahitaji kuwa sehemu ya kikosi cha kimataifa.
 
Pia nakwenda Mali kuhakikisha kwamba kutakuwa na mazungumzo ya kisiasa - kwa vile sasa imewakimbiza wapiganaji - mazungumzo ya kutafuta utulivu na mkataba wa amani."

No comments:

Post a Comment