Friday 25 January 2013

Tume ya Mabadiliko ya Katiba Imeshindwa kwenda na wakati

Nicodemus Minde
Tupo kwenye zama za teknolojia na utandawazi. Mambo yote maisha ya mwanadamu siku hizi yanafanya kutumia ujumuiko wa watu wote duniani. Jumuiya ya dunia kwasasa inaletwa pamoja na mbinu za kisasa ambazo hujuisha mambo kama matumizi ya wavuti, mitandao ya kijamii, tarakilishi, barua pepe na kadhalika. Matumizi haya yamesaidia sana katika ukuzaji na ukuzwaji wa biashara, taasisi mbali mbali, mashirika yasio ya kiserakali, asasi za dini, taasisi za elimu, mashirika ya kijamii. Mashirika haya pamoja na asasi hizi zimetumia jukwaa hili la utandawazi kupanuka kibiashara, kitaasisi, kijamii na kadhalika. Upanuzi huu umesaidia makampuni haya na taasisi hizi kujiuza na kuhabarisha na kusambaza habari kuhusiana na taarifa zao, hoja zao na kadhalika.

Nimeshangazwa na tovuti ya tume ya mabadiliko ya katiba Tanzania kutofuata mkondo huu ilikusaidia kuhabarisha umma ya Tanzania pamoja na jamii nzima ya kimataifa kuhusiana na maendeleo yao katika mchakato mzima wa kukusanya maoni, taarifa za tume na mambo mengine yanayohusu tume hio.
 
Tovuti rasmi ya tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Tanzania imeshindwa kutoa habari muhimu zinazohusu maoni ya vyama, maoni ya taasisi mbali mbali, maoni binafsi na hata wameshindwa kuwa na kipengele (link) ya habari zinazotokana na maoni ya katiba, taarifa zitokanzo na mchakato wa katiba na hata mienendo mbali mbali ya Katiba katika mataifa mbali mbali.

Rai yangu ni kwa tume hii. Taarifa ni kitu muhimu sana katika mchakato wa kuandaa katiba. Kuna haja kubwa kwa tume hii kuweka taarifa muhimu zitokanazo na maoni kuhusu katika. Nimefurahishwa na vipengele vilivyowekwa kwenye tovuti yao. Sheria kuhusu mabadiliko ya katiba imewekwa ndani, katiba ya sasa pia imewekwa ndani, pamoja na muundo wa tume hio inayoongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu Joseph Warioba. 

Tovuti inapaswa kujumuisha madhalani maoni kuhusiana na muundo wa nchi, maoni kuhusiana na Muungano, sera mbali mbali za chama, mustakabali wa maendeleo ya mchakato huu. Misingi ya maendeleo ambalyo ndio chimbuko la mchakato huu wa mabadiliko ya katika inajumuisha azma ya upanuzi wa matumizi ya teknojia, upasishaji habari, kuleta watu pamoja na kadhalika.

Hii ndio rai yangu.

No comments:

Post a Comment

[ZELEZA] Malawi’s Political Earthquake: Nullification of the Presidential Elections

By Prof Paul Tiyambe Zeleza  3/2/2020 The Malawian Constitutional Court has annulled last year's presidential election results....

Most Viewed