Friday, 26 October 2012

Bensouda afika Rift Valley kwa upelelezi zaidi

Kwa hisani ya VOA Swahili na Binafsi
 
October 26, 2012: Mwendesha mashtaka mkuu katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC, Fatou Bensouda, amekamilisha mazungumzo yake nchini Kenya na Rais wa nchi hiyo Mwai Kibaki, Waziri Mkuu Raila Odinga, Jaji Mkuu pamoja na viongozi wengine wa juu katika serikali ya mpito.

Bi, Bensouda pia  alianza kuchukua maoni Jumatano ya waathirika wa ghasia na mauaji yaliyotokea katika uchaguzi mkuu uliopita nchini humo kabla ya kuelekea katika miji ya Naivasha, Nakuru na Eldoret katika jimbo la Rift Valley ili kukutana ana kwa ana na baadhi ya waathirika wa ghasia hizo.
 
Ujio wa Bi. Bensouda nchini Kenya unaashiria nia ya Mahakama hio iliyopo Hague kwamba ipo makini na inakusudia kuleta haki kwa waathirika wa machafuko ya mwaka 2007. Bensouda amekutana na mashirika ya kiraia pamoja na wahanga ya machafuko. 

Kesi zinazowahusu wahusika wakuu kama vile Makamu Waziri Mkuu Uhuru Kenya, waziri wa zamani na mbunge wa Eldoret Kaskazini William Ruto na wengine wawili inatarajia kuanza Aprili mwaka ujao.

No comments:

Post a Comment