Monday, 30 July 2012

Mwanariadha Mchina, Daktari Mtanzania: Yupi Bora?

Nicodemus Minde

Kati ya mambo muhimu katika dunia kwasasa ni michezo. Juzi hapa tumeshuhudia ufunguzi mkali wa Michezo ya Olympic pale jijini London. Zilikua sherehe za kufana na zinazothibitisha michezo kama mhimili wa uchumi. Siku ya pili tu kwenye mashindano haya, tumeshuhudia msichana mdogo wakichina Ye Shiwen mwenye umri wa miaka 16 akivunja rekodi ya dunia kwenye mashindano ya kuogelea ya Medley. Magazeti mengi ya dunia na blog nyingi za kispoti zilijazwa na taarifa ya msichana mdogo akivunja rekodi ya dunia na kuiletea nchi yake dhahabu. Msichana huyo ambaye anatoka katika mkoa wa pwani mashariki wa  Zhejiang alichukua muda wa 4:28.43 kushinda. MV Bukoba ilivyokua inazama mwaka wa Mei 1996, msichana huyu alikua hajazaliwa. Tanzania, kwa wakati huo ilikua inatimiza miaka 35 ya uhuru. Mwaka huo pia Tanzania ilipeleka kikosi cha wanariadha kwenye Olympic ya mwaka 1996 kule Atlanta. Tulitoka kapa. Mara ya mwisho kwa Tanzania kushinda medali ilikua mwaka wa 1980 kule Moscow ambapo wanariadha Filbert Bayi na Suleiman Nyambui walishinda medali za fedha kwenye riadha.

Tathmini yangu ni kwamba Taifa letu limeamua kutotilia maanani umuhimu wa michezo. Licha ya hilo, wazazi wetu wanazingatia mno suala la elimu huku wakidharau michezo. Utamsikia mzazi akimwambia mwanaye "Soma kwa bidii uwe daktari" ama "Achana na upumbavu wa kuota kuwa muogeleaji, kwani umekua samaki?" Hapo ndipo wengi tunakosea. Michezo kwa wenzetu wa Ulaya umekua kama ajira. Michezo imejenga uchumi wa mataifa mengi. Leo hii, Tanzania tunaweka kipau mbele mambo mengi yasiyo na msingi. Huyu msichana wa Kichina na umri wake mdogo, amejishindia medali, maelfu ya dola, umaarufu, na maofa kibao. Akirudi kwao China, kampuni nyingi za vinywaji baridi vitamfuata wakitaka auze bidhaa zao. Utamuona kwenye matangazo mengi kwenye runinga zenu, kwenye magezeti na hata kwenye mitandao. Sisemi kusomea udaktari ama uhandisi ni vibaya. Ni wakati muafaka kwa Tanzania kuanza kufukiria swala la kupanua wigo la uchumi wake. Sio kuzingatia tu kazi za ofisini. 

Tanzania bila michezo haiwezekani!   

No comments:

Post a Comment

[ZELEZA] Malawi’s Political Earthquake: Nullification of the Presidential Elections

By Prof Paul Tiyambe Zeleza  3/2/2020 The Malawian Constitutional Court has annulled last year's presidential election results....

Most Viewed